Rais Trump aliondokana na sera iliyokuwepo ya Magharibi mapema mwezi huu kwa kumpigia simu Rais Putin ili kujadili jinsi ya kumaliza mzozo wa Ukraine, wito uliosifiwa na Moscow kama unaomaliza miaka mitatu ya kutengwa kwa kiongozi huyo wa Kremlin toka aanzishe mashambulizi yake kamili Februari 2022.
Maafisa wakuu wa Russia, na Marekani walikutana Saudi Arabia wiki iliyopita kujadili kurejeshwa kwa uhusiano na kuanza uwezekano wa majadiliano ya kusimamishwa mapambano Ukraine, yote hayo yakifanyika bila kualikwa kwa Kyiv ama Ulaya.
“Haya ni mazungumzo ya marais wawili makini kabisa,” msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov aliiambia televisheni ya serikali Jumapili.
Forum