Israel ilifanya mashambulizi makubwa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, Januari 21, siku mbili baada ya kusitisha mapigano ambayo yalisimamisha vita Gaza, na kisha kuyapanua kujumuisha maeneo mengine ya karibu.
Israel inasema imedhamiria kukomesha wanamgambo katika eneo hilo, lakini Wapalestina wanaona uvamizi huo kama sehemu ya juhudi za kuimarisha udhibiti wa Israel katika eneo hilo, ambapo Wapalestina milioni 3 wanaishi chini ya utawala wa kijeshi.
Uvamizi huo umekuwa mbaya na kusababisha uharibifu kwa maeneo ya mijini na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Forum