Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 00:27

Myanmar na Russia zaingia mkataba wa ushirikiano


Myanmar na mshirika wake wa karibu Russia, walitia saini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji katika eneo maalum la kiuchumi la Dawei, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bandari na kiwanda cha kusafisha mafuta, Wizara ya Maendeleo ya Uchumi ya Russia, imesema Jumapili.

Hati hiyo ilitiwa saini na mkuu wa wizara ya Russia, Maxim Reshetnikov, na waziri wa uwekezaji na uhusiano wa kiuchumi wa Myanmar, Kan Zaw, wakati wa ziara ya ujumbe wa Russia, katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.

“Hati ya mkataba ina vipengele vya msingi vya miradi kadhaa mikubwa ya miundombinu na nishati ambayo inatekelezwa kwa pamoja na makampuni ya Krussia nchini Myanmar, wizara ya Russia, ilimnukuu Reshetnikov akisema katika taarifa.

Ameongeza kuwa wanazungumza kuhusu miradi ya kujenga bandari, mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe na kiwanda cha kusafisha mafuta.

Forum

XS
SM
MD
LG