Biya amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo minne na hajasema iwapo yupo tayari kuondoka au atagombea mhula mwingine katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Raia wengi wa Cameroon, wakiwemo wanasiasa wa upinzani, hawana uhakika iwapo Biya, ambaye aliingia madarakani mwaka 1982, atagombea mhula wa nane katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Biya ameongoza Cameroon kwa mkono wa chuma baada ya uchaguzi wa mwaka 2018 uliokuwa na upinzani mkali na ambao matokeo yake yalipingwa na upinzani.
Wapinzani wake wamekamatwa na kufungwa jela, huku wanaharakati wakisema kumekuwepo na ukandamizaji mkubwa wa haki za kibinadamu.
Kuna wasiwasi kuhusu hali ya afya ya Biya, hasa baada ya kukosa kuonenaka hadharani kwa wiki kadhaa mwaka uliopita.
Forum