Jimbo la Carlifornia linatarajia Dhoruba ya mvua ambayo huenda ikasababisha mafuriko katika sehemu hiyo iliyoharibiwa hivi karibuni na moto.
Idhara ya hali ya hewa ya kitaifa imesema theluji nzito inatarajiwa katika sehemu za Virginia, na west Virginia leo Jumatano.
Dhoruba ya mnvua inayotajwa kama mto hewani, inatarajiwa kusababisha mafuriko baadaye leo Jumatano katika jimbo la Carlifonia na huenda sehemu za mijini Katikati na kusini mwa Carlifonia zikafurika kwa maji
Dhoruba ya theluji iliyoshuhudiwa katika majimbo ya Katikati mwa Marekani, jana Jumanne, ilisababisha ajali kutokana na Barabara kuwa na barafu, n ahata kusababisha shule kufungwa.
Watu 12,000 walikosa umeme katika jimbo la Virginia, jana Jumanne.
Forum