Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Huko Tanzania matokeo ya kitaifa ya mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili kwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2022 yameshuka ikilinganishwa na 2021 Wadau wamewataka wazazi wajihusishe zaidi katika maisha ya watoto wao.
Rais Ruto pia alisema serikali yake tayari inafanya kazi kuwasaidia vijana nchini Kenya kujikwamua kimaisha kupitia program aliyoizindua hivi karibuni inayojulikana kama Husler Fund
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.