Radio
Kenya kutumia vyama vya Sacco kutoa mikopo ya 'Hustler Fund'
Utawala wa Rais William Ruto unapanga kutoa fedha za Hustler Fund kupitia vyama vya mikopo maarufyu Sacco. Katika rasimu ambayo imetolewa hivi punde ya Taarifa ya Sera ya Bajeti ya 2023 (BPS), serikali inapanga kutumia mfumo huo kuimarisha mradi huo unaotarajiwa kuwafaida zaidi vijana.
UN inasema walinda amani waligundua makaburi ya halaiki mashariki mwa DRC
Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kwamba kaburi moja katika kijiji cha Nyamamba lilikuwa na miili 42 wakiwemo watoto sita. Miili saba iligunduliwa katika kaburi moja kwenye kijiji cha Mbogi
Serikali Marekani yafikia ukomo wa kiwango cha kukopa
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema Marekani imefikia kikomo cha kukopa sasa cha dola trilioni 31.4 hivyo basi kuzidisha vita vya kisiasa kati ya Wademokrats na Warepublikan mjini Washington. Warepublikan wakitaka mazungumzo na rais juu ya makubaliano ya kuongeza ukomo wa kukopa.