Mashambulizi yanayoongezeka yamezikumba hospitali na miundombinu mingine ya kiraia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mapigano yanaendelea dhidi ya serikali na kundi la M23, shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu limesema.
Majeshi ya Wanamaji ya Iran, Russia na China yatafanya mazoezi ya katika pwani ya Iran wiki hii katika jitihada za kuimarisha ushirikiano, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti Jumapili.
Marekani imekataa kuendelea na msamaha ulioiruhusu Iraq kununua umeme kutoka Iran bila kukiuka vikwazo, afisa wa Marekani amesema Jumapili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, atawasili Jeddah, Saudi Arabia, Jumatatu kwa mazungumzo kati ya Marekani na Ukraine huku Rais Donald Trump, akishinikiza kumalizika haraka kwa vita vya Russia na Ukraine.
Mtu mwenye silaha anayeaminika alisafiri kutoka Indiana alipigwa risasi na maafisa wa Idara ya Ulinzi wa Viongozi ya Marekani, “U.S. Secret Service,” karibu na White House baada ya makabiliano mapema Jumapili, kulingana na mamlaka.
Ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi na idara ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wanawake na usawa wa jinsia imegundua kuwa karibu robo moja ya serikali kote duniani zimeripoti kuzorota kwa haki za wanawake mwaka jana.
Serekali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatoa zawadi ya dola milioni tano kwa atakaye saidia kuwakamata viongozi wa kundi la M23 ambalo limeteka miji miwili mikubwa ya majimbo ya Kivu, Wizara ya sheria imetangaza.
Kiongozi wa waasi wa Kihouthi wa Yemen, Ijuma amesema kundi hilo litarudia operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel, endapo Israel haitaondoa kizuizi cha misaada cha Gaza ndani ya siku nne.
Kimbunga Alfred kilidhoofika kitropiki Jumamosi kilipokaribia kuwa mvua na upepo uliovuma pwani ya mashariki mwa Australia ambapo mamia ya maelfu ya nyumba hazikuwa na umeme.
Maelfu ya wanawake waliandamana katika mitaa ya miji ya Uturuki Jumamosi kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kupinga ukosefu wa usawa na unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Tanzania imeungana na mataifa mengine ulimwenguni kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake, maadhimisho ya kitaifa yakifanyika mkoani Arusha. Katika maadhimisho hayo, wanawake wameitaka serikali kuendelea kuboresha huduma za afya, hasa kwa wanawake wenye umri mkubwa.
Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika ,(CDC Africa) kimesema Alhamisi kwamba wimbi jipya la maambuziki ya Ebola limezuka Uganda na kwamba juhudi zinafanywa ili kuongeza ufuatiliaji wa maambukizi.
Pandisha zaidi