Papa Francis yuko katika hali ya utulivu anapopambana na niumonia hospitalini kwa siku ya 17 sasa, na anapumzika baada ya kuwa na usiku wa amani, Vatican imesema Jumapili.
Meli ya kubeba ndege ya Marekani, imewasili Korea Kusini, Jumapili katika kuonyesha uwepo wa nguvu ya kijeshi, siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ili kuonyesha uwezo wake wa kukabiliana na mashambulizi.
Uingereza, Ufaransa na Ukraine zimekubaliana kufanyia kazi mpango wa kusitisha mapigano kuwasilishwa kwa Marekani, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, amesema Jumapili alipokuwa akijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa Ulaya kujadili kumaliza vita.
Israel imesitisha kuingia kwa bidhaa na vifaa katika Ukanda wa Gaza, Jumapili na kuonya kuhusu matokeo ya ziada ikiwa kundi la Hamas ambalo limetajwa kuwa la kigaidi na Marekani, halitakubali pendekezo jipya la kurefusha usitishaji mapigano.
Maafisa wa Vatican Jumamosi wamesema Papa Francis alipumzika kwa amani baada ya kupata shida ya kupumua Ijumaa.
Moscow Jumamosi imesema imeteka vijiji viwili zaidi mashariki mwa Ukraine huku maafisa wa Kyiv wakisema kuwa mashambulizi ya Russia yameua mtu mmoja na kujeruhi 19.
Awamu ya kwanza ya mapatano ya Israel na Hamas inamalizika Jumamosi, na mazungumzo juu ya hatua inayofuata ya kupata usitishaji wa kudumu wa mapigano, hadi sasa hayajakamilika.
Mkutano uliofanyika White House kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Ijumaa uliolenga kufikia makubaliano ambayo huenda yatairuhusu Marekani kupata haki ya madini nadra ya Ukraine uligeuka kuwa ni malumbano.
Waislamu sehemu mbali mbali duniani wanajitayarisha kuuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuangalia mwezi, kuanza ibada hadi ununuzi wa bidhaa za kutumia mwezi huu.
Maelfu ya watu walikusanyika katika miji kote Ugiriki siku ya Ijumaa kudai haki yao wakati wa kumbukumbu ya mwaka wa pili wa ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea nchini humo, huku wafanyakazi waliogoma wakisimamisha safari za ndege na usafiri wa baharini na treni.
Mahakama ya Juu ya Namibia siku ya Ijumaa ilitupilia mbali pingamizi dhidi ya uchaguzi wa rais wa mwaka jana lililowasilishwa na vyama vya upinzani, hatua ambayo inampa nafasi Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama kinachotawala, kuwa rais kuanzia mwezi ujao.
Shirika la serikali ya Marekani linalosimamia vyombo vya habari vinavyorusha matangazo kote duniani, USAGM, Alhamisi limetangaza kuwa mwanahabari aliyegeuka mwanasiasa Kari Lake atajunga na shirika hilo kama mshauri maalum.
Pandisha zaidi