Wanajeshi wa Sudan kusini wamezingira makao ya makam rais Riek Machar katika mji mkuu wa Juba.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya sasa, Wamarekani wengi zaidi wanaamini kuwa nchi yetu inaelekea kwenye mwelekeo sahihi kuliko mwelekeo mbovu – katika rekodi ya kushangaza ya pointi 27 tangu siku ya uchaguzi.
Canada, Mexico na China Jumanne wote wamesema kwamba wataweka ushuru wa majibu kwenye bidhaa kutoka Marekani kufutia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuweka ushuru mpya kwa bidhaa zao zinazoingia Marekani.
Marekani imeweka bayana kwamba haitakuwa ikitoa mchango wa moja kwa moja kwa majukwaa ya Umoja wa Mataifa yakiwemo maendeleo endelevu pamoja na malengo mengine ya kimataifa ikijumuisha kutokomeza umaskini, katika upigaji kura kwenye Baraza Kuu la Umoja huo Jumanne.
Utabiri wa hali ya ukame katika mzunguko ujao wa mazao unatarajiwa kuwasukuma watu wengine zaidi ya milioni moja katika kiwango cha mzozo wa njaa nchini Somalia katika miezi ya hivi karibuni
Rais Donald Trump amekuwa wazi kwamba anazingatia amani, afisa wa ngazi ya juu wa utawala ameiambia VOA katika barua pepe.
Maelfu ya wakimbizi katika kambi hiyo ni watu wanaokimbia vita na ukame katika nchi jirani za Sudan Kusini, Ethiopia, Burundi na Congo
Zaidi ya Wakenya 60 waliookolewa kutoka mikononi mwa makundi ya matapeli wa mtandaoni nchini Myanmar wamekwama kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand wakiishi katika mazingira mabaya, kulingana na taifa hilo la Afrika Mashariki.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF Jumatatu limeonya kuwa uamuzi wa Israel wa kuzuia upelekaji wa misaada ya kibinadamu isipokuwa maji kwenye Ukanda wa Gaza, kwa haraka utapelekea hatari kubwa kwa watoto na familia ambazo tayari zimetatizika.
Kampuni kubwa ya kutengeneza chips za kompyuta ya Taiwan Semiconductor Manufacturing, au TSMC Jumatatu imetangaza kuongeza uwekezaji wa dola bilioni 100 hapa Marekani kwa kujenga viwanda 5 zaidi vya kutengeneza chips ndani ya miaka kadhaa ijayo.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kwamba hakuna matumaini kwamba Mexico na Canada wataepuka ushuru wa asilimia 25 unaoanza kutozwa le Jumanne, na hivyo kulitikisa soko la fedha kutokana na vizingiti vipya vya biashara na Marekani.
Pandisha zaidi