Shirika la mpango wa chakula ulimwenguni limesema Jumatatu, likionya kwamba idadi inaweza kuongezeka kutokana na kupunguzwa ufadhili.
Mwaka 2022 pembe ya Afrika ilikabiliwa na hali mbaya ya ukavu katika kipindi cha zaidi ya miongo minne baada ya mvua kutonyesha na kusababisha vifo vya watu takriban elfu 43 kwa mujibu wa utafiti .
Ripoti ya karibuni inakadiria kwamba takriban watu milioni 3.4 wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula nchini Somalia.
Hata hivyo hii itaongezeka kufikia milioni 4.4 katika miezi ya karibuni , mkurugenzi wa WFP wa huduma ya uchambuzi wa usalama wa chakula na lishe Jean Martin Bauer amesema akimaanisha awamu ya tatu na zaidi katika mfumo wa uainishaji wa awamu ya usala wa chakula.
Njaa imeathiri sana watoto na kwa mujibu wa makadirio ya sasa Watoto milioni 1.7 walio chini ya umri wa miaka mitano wanauwezekano wa kupata utapiamlo ifikapo Desemba mwaka 2025, WFP imesema.
Forum