Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu alisema Alhamisi kwamba Ufaransa inashirikiana taarifa za kijasusi na Ukraine, hatua iliyofuatia baada ya Marekani kusema inapunguza ushirikiano wa kijasusi na Ukraine.
Hamas iliyotajwa kuwa kundi la kigaidi na Marekani ilisema Alhamisi kwamba vitisho kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump vinahimiza Israel iondoke kwenye makubaliano ya usitishaji mapigano huko Gaza.
Iran imekamilisha miezi miwili ya mazoezi makali ya kijeshi katika miongo kadhaa huku ikijaribu kuzuia uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa mahasimu wake Israel na Marekani, watafiti wa usalama wameiambia VOA.
Wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakijiandaa kwa mazungumzo ya dharura kuhusu misaada ya kijeshi baada ya utawala wa Trump kusitisha msaada wake kwa Ukraine, wataalam kadhaa wa Russia wanasema kuwa Moscow inajitahidi kuvuruga mshikamano wa Magharibi.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano amechelewesha kwa mwezi mmoja ushuru mpya wa asilimia 25 kwa magari kutoka Mexico na Canada wakati kukiwa na wasi wasi kwamba vita vya biashara na mataifa hayo jirani huenda vikawaumiza watengenezaji watatu wakubwa wa magari nchini Marekani.
Wanajeshi wa Sudan kusini wamezingira makao ya makam rais Riek Machar katika mji mkuu wa Juba.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya sasa, Wamarekani wengi zaidi wanaamini kuwa nchi yetu inaelekea kwenye mwelekeo sahihi kuliko mwelekeo mbovu – katika rekodi ya kushangaza ya pointi 27 tangu siku ya uchaguzi.
Canada, Mexico na China Jumanne wote wamesema kwamba wataweka ushuru wa majibu kwenye bidhaa kutoka Marekani kufutia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuweka ushuru mpya kwa bidhaa zao zinazoingia Marekani.
Marekani imeweka bayana kwamba haitakuwa ikitoa mchango wa moja kwa moja kwa majukwaa ya Umoja wa Mataifa yakiwemo maendeleo endelevu pamoja na malengo mengine ya kimataifa ikijumuisha kutokomeza umaskini, katika upigaji kura kwenye Baraza Kuu la Umoja huo Jumanne.
Utabiri wa hali ya ukame katika mzunguko ujao wa mazao unatarajiwa kuwasukuma watu wengine zaidi ya milioni moja katika kiwango cha mzozo wa njaa nchini Somalia katika miezi ya hivi karibuni
Rais Donald Trump amekuwa wazi kwamba anazingatia amani, afisa wa ngazi ya juu wa utawala ameiambia VOA katika barua pepe.
Pandisha zaidi