Serikali ya Tanzania siku ya Alhamisi, imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg baada ya siku 42 bila kuwepo na maambukizi mapya, hatua inayokidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano kwenye Ikulu ya Marekani amekutana na Waziri Mkuu wa Ireland Michael Martin wakati wakifanya mazungumzo mapana kuanzia tofauti za kibiashara hadi mzozo wa Gaza, ingawa wote waliahidi kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Jumatano ametupilia mbali wazo la kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu mkataba wa nyuklia, baada ya kupokea barua kutoka kwa Rais Donald Trump ambaye alipendekeza mazungumzo hayo.
Jumuia ya maendeleo ya Afrika Mashariki Jumatano ilionya kwamba mapigano ya hivi karibuni nchini Sudan Kusini yanaipeleka nchi hiyo “kwenye hatari ya kurudi katika vita.”
Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yataanza katika mji mkuu wa Angola tarehe 18 Machi, ofisi ya rais wa Angola ilisema Jumatano katika taarifa.
Vita vya kibiashara vya Marekani na Canada na Umoja wa Ulaya vilishika kasi Jumatano, huku Rais Donald Trump na washirika wa Marekani wakiwekeana ushuru mpya.
Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, William O’Neil Jumanne ameambia wanahabari mjini New York kwamba hali ya kiusalama nchini humo ni tete huku akisihi wahusika wa kitaifa na kimataifa kuheshimu haki za binadamu.
Maafisa wa Ufilipino wanasema Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekamatwa Rodrigo Duterte aliondoka mjini Manila akiwa ndani ya ndege na atakabidhiwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini The Hague.
Angola Jumanne ilisema itajaribu kuanzisha katika siku zijazo mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 ambao inasemekana wanaoungwa mkono na Rwanda.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne alasiri alibadili msimamo kuhusu tishio lake la kuongeza maradufu ushuru kwenye chuma na aluminum kutoka Canada.
Maafisa wa Marekani na Ukraine walikutana Jumanne mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa mazungumzo kuhusu juhudi za kumaliza vita kati ya Russia na Ukraine, huku pande zote mbili zikisema Kyiv inaunga mkono mpango wa Marekani wa sitisho la mapigano kwa siku 30.
Pandisha zaidi