Sumy iko katika mpaka kutoka mkoa wa Kursk nchini Russia ambako vikosi vya Ukraine vilianzisha mashambulizi mwezi Agosti.
Wakati huo huo Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema ni watu wa Taiwan pekee wanaoweza kuamua mustakabali wao.
Papa Francis alifuatilia ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video siku ya Jumapili.
Tukio limetokea saa chache baada ya wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani kuanza mazoezi yao ya pamoja ya kila mwaka.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ambaye afya yake imeendelea kuimarika wakati akipokea matibabu kutokana na homa ya mapafu, Jumapili aliwashukuru madaktari pamoja na wahudumu wa afya, ingawa hakuweza kuongoza maombi ya Angelus kwa mara ya nne mfululizo.
Mark Carney, ambaye hivi karibuni atakuwa waziri mkuu mpya wa Canada, ni gavana wa zamani wa benki kuu ya Canada na ile ya Uingereza, atakabiliwa na kibarua kigumu cha kuiongoza Canada chini ya ushuru wa ziada uliowekwa na Rais Donald Trump.
Maafisa wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump wamemkamata mwanafunzi raia wa Palestina aliyehitimu ambaye alihusika sana katika maandamano ya Wapalestina ya mwaka jana katika chuo kikuu cha Columbia cha New York, chama cha wanufunzi kilisema Jumapili.
Israel Jumapili ilitangaza kwamba imekata huduma ya umeme kwa Gaza. Matokeo ya hatua hiyo hayakueleweka haraka, lakini eneo la Gaza linapata umeme kutoka Israel ili kuzalisha maji ya kunywa.
Mashambulizi yanayoongezeka yamezikumba hospitali na miundombinu mingine ya kiraia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mapigano yanaendelea dhidi ya serikali na kundi la M23, shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu limesema.
Majeshi ya Wanamaji ya Iran, Russia na China yatafanya mazoezi ya katika pwani ya Iran wiki hii katika jitihada za kuimarisha ushirikiano, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti Jumapili.
Marekani imekataa kuendelea na msamaha ulioiruhusu Iraq kununua umeme kutoka Iran bila kukiuka vikwazo, afisa wa Marekani amesema Jumapili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, atawasili Jeddah, Saudi Arabia, Jumatatu kwa mazungumzo kati ya Marekani na Ukraine huku Rais Donald Trump, akishinikiza kumalizika haraka kwa vita vya Russia na Ukraine.
Pandisha zaidi