Akiwa Jeddah, Rubio pia atakutana na Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman Al Saud, kujadili njia za kuendeleza maslahi ya pamoja katika eneo hilo na kuimarisha uhusiano wa Marekani na Saudia, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Tammy Bruce.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Rubio “amesisitiza azma ya Rais Trump ya kumaliza vita haraka iwezekanavyo na kusisitiza kwamba pande zote lazima zichukue hatua ili kupata amani endelevu,” katika simu ya Ijumaa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha.
Jumatatu, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy atakwenda kwenye ufalme wa Ghuba kwa mkutano na Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman.
Forum