Msamaha wa awali uliisha Jumamosi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haikuurejesha upya, ubalozi wa Marekani wa Baghdad umesema katika taarifa.
Uamuzi huo umefanyika ikiwa sehemu ya “kampeni ya shinikizo la juu” la Rais Donald Trump dhidi ya Iran, ambayo “imewekwa kumaliza tishio la nyuklia la Iran, kupunguza mpango wake wa makombora ya masafa ya mbali, na kuizuia kuunga mkono vikundi vya kigaidi,” imesema taarifa hiyo.
“Tunaitaka serikali ya Iraq iondoe utegemezi wake kwa vyanzo vya nishati vya Iran haraka iwezekanavyo, na kukaribisha ahadi ya Waziri Mkuu wa Iraq, ya kufikia uhuru wa nishati,” imesema taarifa hiyo.
Licha ya utajiri wake wa mafuta na gesi, Iraq imekumbwa na uhaba wa umeme kwa miongo kadhaa kwa sababu ya vita, ufisadi na usimamizi mbovu na imekuwa ikitegemea sana gesi na umeme kutoka Iran.
Forum