Wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda wamepiga hatua kubwa katika eneo hilo toka Januari, wakiteka miji muhimu ya Goma na Bukavu na kuwafanya maelfu ya watu kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
“Kati ya Machi 1 na 3, hospitali kadhaa zililengwa na wenye silaha katika kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vituo vya matibabu na wafanyikazi wa afya,” Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika ripoti iliyochapishwa Jumamosi.
Usalama Goma unatishiwa baada ya kuzuka upya kwa vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na wizi mjumbani, huku hospitali na shule zikilazimika kufungwa katika maeneo mengine.
Forum