Serekali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatoa zawadi ya dola milioni tano kwa atakaye saidia kuwakamata viongozi wa kundi la M23 ambalo limeteka miji miwili mikubwa ya majimbo ya Kivu, Wizara ya sheria imetangaza.
Kiongozi wa waasi wa Kihouthi wa Yemen, Ijuma amesema kundi hilo litarudia operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel, endapo Israel haitaondoa kizuizi cha misaada cha Gaza ndani ya siku nne.
Kimbunga Alfred kilidhoofika kitropiki Jumamosi kilipokaribia kuwa mvua na upepo uliovuma pwani ya mashariki mwa Australia ambapo mamia ya maelfu ya nyumba hazikuwa na umeme.
Maelfu ya wanawake waliandamana katika mitaa ya miji ya Uturuki Jumamosi kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kupinga ukosefu wa usawa na unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Tanzania imeungana na mataifa mengine ulimwenguni kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake, maadhimisho ya kitaifa yakifanyika mkoani Arusha. Katika maadhimisho hayo, wanawake wameitaka serikali kuendelea kuboresha huduma za afya, hasa kwa wanawake wenye umri mkubwa.
Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika ,(CDC Africa) kimesema Alhamisi kwamba wimbi jipya la maambuziki ya Ebola limezuka Uganda na kwamba juhudi zinafanywa ili kuongeza ufuatiliaji wa maambukizi.
Rais wa Marekani Donald Trump Alhamisi amethibitisha kwamba utawala wake unafanya mashauriano na kundi la Hamas ambalo limeorodheshwa na Marekani ni la kigaidi.
Rais wa Marekani Donald Trump Alhamisi amechelewesha kwa wiki nne ushuru mpya wa asilimia 25 kwenye bidhaa nyingi kutoka Mexico na Canada kwa mauzo yake kuja Marekani.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu alisema Alhamisi kwamba Ufaransa inashirikiana taarifa za kijasusi na Ukraine, hatua iliyofuatia baada ya Marekani kusema inapunguza ushirikiano wa kijasusi na Ukraine.
Hamas iliyotajwa kuwa kundi la kigaidi na Marekani ilisema Alhamisi kwamba vitisho kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump vinahimiza Israel iondoke kwenye makubaliano ya usitishaji mapigano huko Gaza.
Iran imekamilisha miezi miwili ya mazoezi makali ya kijeshi katika miongo kadhaa huku ikijaribu kuzuia uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa mahasimu wake Israel na Marekani, watafiti wa usalama wameiambia VOA.
Wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakijiandaa kwa mazungumzo ya dharura kuhusu misaada ya kijeshi baada ya utawala wa Trump kusitisha msaada wake kwa Ukraine, wataalam kadhaa wa Russia wanasema kuwa Moscow inajitahidi kuvuruga mshikamano wa Magharibi.
Pandisha zaidi