Utabiri wa hali ya ukame katika mzunguko ujao wa mazao unatarajiwa kuwasukuma watu wengine zaidi ya milioni moja katika kiwango cha mzozo wa njaa nchini Somalia katika miezi ya hivi karibuni
Rais Donald Trump amekuwa wazi kwamba anazingatia amani, afisa wa ngazi ya juu wa utawala ameiambia VOA katika barua pepe.
Maelfu ya wakimbizi katika kambi hiyo ni watu wanaokimbia vita na ukame katika nchi jirani za Sudan Kusini, Ethiopia, Burundi na Congo
Zaidi ya Wakenya 60 waliookolewa kutoka mikononi mwa makundi ya matapeli wa mtandaoni nchini Myanmar wamekwama kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand wakiishi katika mazingira mabaya, kulingana na taifa hilo la Afrika Mashariki.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF Jumatatu limeonya kuwa uamuzi wa Israel wa kuzuia upelekaji wa misaada ya kibinadamu isipokuwa maji kwenye Ukanda wa Gaza, kwa haraka utapelekea hatari kubwa kwa watoto na familia ambazo tayari zimetatizika.
Kampuni kubwa ya kutengeneza chips za kompyuta ya Taiwan Semiconductor Manufacturing, au TSMC Jumatatu imetangaza kuongeza uwekezaji wa dola bilioni 100 hapa Marekani kwa kujenga viwanda 5 zaidi vya kutengeneza chips ndani ya miaka kadhaa ijayo.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kwamba hakuna matumaini kwamba Mexico na Canada wataepuka ushuru wa asilimia 25 unaoanza kutozwa le Jumanne, na hivyo kulitikisa soko la fedha kutokana na vizingiti vipya vya biashara na Marekani.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye alikuwa na nafasi muhimu katika majadiliano ya makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya mwaka 2015, kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, amejiuzulu kama makamu wa rais, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumatatu.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba nchi yake iko tayari kutia saini mkataba wa madini nyeti na Marekani, na kwamba anaamini kuwa anaweza kuokoa uhusiano uliodorora kati yake na Rais Donald Trump.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badir Abdelatty amesema Jumapili kwamba mpango wa kuikarabati Gaza utakaohakikisha kwamba Wapalestina wanabaki kwenye ardhi yao umekamilika na utawasilishwa kwenye mkutano wa dharura wa mataifa ya Kiarabu Jumanne mjini Cairo.
Hali ya vita vya Russia dhidi ya Ukraine vilivyodumu miaka 3 ilibaki kuwa ya wasiwasi Jumapili wakati Marekani ikisema kwamba haina uhakika amani inaweza kupatikana
Pandisha zaidi