Hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa katika ufyatuaji risasi huo uliotokea usiku wa manane karibu na mtaa kutoka White House, kwa mujibu wa taarifa ya Secret Service.
Rais Donald Trump alikuwa Florida wakati ufyatuaji risasi huo unatokea. Idara hiyo ilipokea taarifa kutoka kwa polisi wa eneo hilo kuhusu madai ya “mtu aliyejiua” ambaye alisafiri kutoka Indiana na walikuta gari la mtu huyo ambalo linalo shabihiana na maelezo yaliyotolewa eneo la karibu.
“Maafisa walipomkaribia, mtu huyo alifyatua bunduki na makabiliano ya silaha yakatokea, ambapo risasi zilifyatuliwa na wafanyakazi wetu,” Idara ya “Secret Service,” imesema katika taarifa.
Forum