Pia inaeleza ubaguzi bado umejikita katika uchumi na jamii.
Licha ya baadhi ya maendeleo, ikiwemo elimu kwa wasichana na fursa kwa uzazi wa mpango, UN Women imesema mwanamke au msichana anauawa kila dakika 10 na mshirika au mwana familia na kwamba kesi za manyanyaso ya ngono yanayohusiana na mizoz zimeongezeka kwa asilimia 50 tangu mwaka 2022.
Ripoti, ilitolewa kabla ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kesho Jumamosi, pia imeelezea kuwa nchi 87 tu zimewahi kuongozwa na mwanamke.
Katika tathmini mpya, ambayo inajumuisha michango kutoka nchi 159, UN Women imesema nchi zimechukua hatua nyingi kusonga mbele na usawa wa jinsia na haki za wanawake katika muda wa miaka mitano iliyopita lakini haki kama hizo bado zinakabiliwa na ongezeko la vitisho kote duniani.
Mkurugenzi wa Sera na Mpango UN Women
Sarah Hendriks ni Mkurugenzi wa Sera, Mpango wa Idara ya Serikali katika UN Women.
Sarah Hendriks, Mkurugenzi wa Sera, UN Women amesema: “Dunia kwa kweli, inakabiliwa na upinzani unaoongezeka dhidi ya usawa wa jinsia na haki za wanawake.
Wahusika wanaopinga haki ambazo wanazidi kufadhiliwa na kuratibiwa wanadhoofisha kikamilifu maafikiano ya muda mrefu kuhusu masuala muhimu ya haki za wanawake na pale ambapo hawawezi kurudisha nyuma faida za kisheria au sera kwa ujumla, wanajaribu kuzuia au kupunguza kasi ya utekelezaji wao.”
Kwa upande Chanya, ripoti imesema kiasi cha asilimia 88 ya nchi zimepitisha sheria za kupambana dhidi ya wanawake na kuweka huduma za kuwasaidia waathirika katika muda wa miaka mitano iliyopita.
Nchi nyingi zimepiga marufuku ubaguzi kwenye maeneo ya kazi, na asilimia 44 wanaboresha ubora wa elimu na mafunzo kwa wasichana na wanawake, imesema.
Hendriks ameongeza kuwa: “Habari njema ni kwamba dunia hivi leo kwa hakika ina usawa zaidi kwa wanawake na wasichana kuliko ilivyokuwa hapo kabla, na hiyo inabainisha maendeleo, kwa kweli, yanawezekana.
Ripoti ya UN Inatoa Data na Ushahidi
Na bado, ripoti pia inaonyesha, kwa data na ushahidi, maendeleo yamekuwa ya pole pole sana, na nyeti, yasiyo na uwiano, na lililo muhimu sana, kuwa maendeleo haya hayana uhakikisho.”
Bado ubaguzi umejikitia sana, huku kukiwa na mianya katika madaraka na rasilimali ambazo zinaminya haki za wanawake, ripoti imesema
Mkurugenzi huyo wa Sera, UN Women alisema: “Hivyo hivi sasa, msichana ambaye amezaliwa leo atasubiri mpaka akaribie miaka 40 ndipo atakapoona usawa katika mabunge kila mahali, kuna ukosefu wa usawa katika mabunge.
Atakuwa na miaka 68 mpaka ndoa za mapema kwa wasichana zitakapomalizwa kote duniani, na wala hataishi aone siku ambayo umaskini uliokithiri, ambao una uso wa mwanamke, umetokomezwa katika ardhi hii. Atakuwa na miaka 137 wakati ambapo umaskini kwa wanawake umetokomezwa.”
Ripoti Inaonya Wadau Wanadumaza Muafaka
Ripoti hiyo imeonya kuwa ‘wadau dhidi ya haki kwa bidii wanadumaza muafaka wa muda mrefu kwa masuala makuu ya haki za wanawake,’ na kutaka kuzuia au kupunguza kai ya kisheria na mafanikio ya sera ambayo hayawezi kurejewa.
Kadhalika inataka mapinduzi ya kidigitali kuhakikisha fursa sawa kwa teknnolojia kwa wote wanawake na wasichana; uwekezaji katika hifadhi ya kijamii, ikiemo huduma ya afya kwa wote na usawa wa elimu ili kuwaondoa katika umaskini; na hakuna manyanyaso dhidi ya wasichana na wanwake. Mchakato pia utajumuisha usawa katika kufanya maamuzi ya madaraka kwa wanawake na kufadhili majibu ya misaada ya kibinadamu kijinsia’ katika vita na mizozo.
Forum