Radio
19:30 - 19:59
Mapigano nchini Sudan yaingia siku ya sita huku maelfu wakiondoka Khartoum wakihofia usalama wao.
Makombora, mashambulizi ya anga na milio ya risasi yameendelea bila ya kusita mjini Khartoum tangu Jumamosi pale mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan akipigana vita na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza kikosi cha usaidizi wa haraka cha wanamgambo, RSF.
21:00 - 21:29
Mawaziri wa Uganda waanza kurejesha mabati waliyogawana ya watu wa Karamoja.
Serikali ya Uganda ilinunua mabati ya kuezekea kwa ajili ya kusambazwa bure kwa watu walio na kipato cha chini na masikini wa eneo la Karamoja lakini maafisa wakuu wa serikali mjini Kampala badala yake waligawana mabati kati yao wenyewe.