Radio
16:30 - 16:59
Kenya imetangaza tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kuwa la kitaifa linalostahili kushughulikiwa kama ugaidi na wizi wa mifugo
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo.
19:30 - 20:29
Livetalk: Dunia yaadhimisha Siku ya Watoto wa Mitaani
Katika Livetalk wiki hii tunajadili maadhimisho ya Siku ya watoto wa Mitaani tukiangazia mafanikio na changamoto zinazoendelea kukumba juhudi za kuboresha hali ya maisha ya watoto wapatao milioni 150 kote duniani ambayo inaelezwa kuathiriwa mno na kupanda kwa gharama ya maisha.