Radio
19:30 - 20:00
Bi Biden ajionea mwenyewe athari za ukame Afrika Mashariki, aahidi 70% ya misaada yote ya kimataifa
Mke wa rais wa Marekani, Jill Biden, Jumapili alipata nafasi ya kujionea kwa karibu hali mbaya ya ukame wa kihistoria unaoshuhudiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Bi. Biden alitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame nchini Kenya, katika kaunti ya Kajiado.