Radio
Kenya: wagombea urais watakiwa kuwasilisha majina ya wagombea wenza hadi May 16
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) baada ya kukutana Jumanne na vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi wa Agosti 9, imetangaza kwamba wanaowania urais watakiwa kuwasilisha majina ya wagombea wenza kwa tume hiyo ifikapo tarehe 16 Mei.
Habari kuhusu ununuzi wa mtandao wa Twitter zaibua hisia mseto
Baada ya kubainiika kwamba bilionea Elon Musk amefikia makubaliano na kampuni ya Twitter kununua mtandao wake wa kijamii, mgawanyiko kati ya mirengo ya kisiasa Marekani imeanza kujidhihirisha huku mrengo wa kulia ukishangilia hatua hiyo na ule wa kushoto ukieleza wasiwasi wake.
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda arejeshwa kutoka Sweden
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari Jean-Paul Micomyiza, aliwasili Kigali, Alhamisi kukabiliana na shutuma zake. Nairobi yawa mwenyeji wa mazungumzo ya serekali ya DRC na makundi ya uasi huku mapigani yakiendelea na M23. WHO imesema vita vya UKraine vimeingilia mpango wa chanjo wa kuokoa maisha.