Radio
06:00 - 06:30
Serikali ya Kenya inasema imerejesha usambazaji wa kawaida wa mafuta ya petroli.
Kenya ilikabiliwa na uhaba wa mafuta kwa wiki kadhaa. Serikali ililaumu makampuni ya mafuta na wafanyabiasha binafasi kuficha bidhaa hiyo ili wanufaike. Sasa Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai imeanzisha uchunguzi dhidi ya waliohodhi mafuta.
21:00 - 21:29
Mzozo wa kibinadamu nchini Ukraine ni changamoto kubwa mno kwa jumuiya ya kimataifa
Umoja wa Mataifa unasema idadi ya wakimbizi kutoka Ukraine imefikia milioni 5 huku wengine milioni 7 wakitafuta hifadhi ndani ya nchi hiyo katika kile kinachoelezwa kama moja ya mizozo mibaya zaidi ya kibinadamu katika historia.