Radio
Askofu Bagonza anasema amefurahishwa na matamshi ya Rais Samia alipoelezea migawanyiko ndani ya nchi
Rais Samia wa Tanzania alisema kuna kazi ya kuirudisha nchi kuwa moja baada ya kutetereka kwa migawanyiko ya udini, ukabila na itikadi. Jambo ambalo limeungwa mkono na askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza
Sintofahamu yaibuka baada ya mamlaka ya mawasiliano Kenya kutangaza usajili rasmi wa laini za simu
Baadhi ya vijana wa Kenya wanalalamikia hali ya sintofahamu iliyoibuliwa na kauli zinazokinzana za Mamlaka ya Mawasiliano (CA) kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu ambazo hazikuwa zimeandikishwa rasmi kabla ya mwaka wa 2015.
Msemaji wa M23 asema kwamba wanataka serikali ya DRC kupambana na makundi mengine ya waasi na kuhakikisha kuna usalama kwa raia
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza kampeni kuelekea duru ya pili ya uchaguzi. msemaji wa waasi wa M23 Mj. Willy Ngoma aambia VOA kwamba ni lazima serikali iheshimu mkataba wa Nairobi na kuhakikisha kwamba inapambana na makundi mengine ya waasi kwa ajili ya usalama wa raia
Mahojiano kamili na msemaji wa kundi la waasi la M23 nchini DRC, Meja Ngoma
Wakati waasi wa M23 wakitangaza kusitisha mapigano kwa sasa, msemaji wao, Willy Ngoma, ameiambia VOA kwamba ni lazima serikali iheshimu mkataba wa Nairobi na kuhakikisha kwamba inapambana na makundi mengine ya waasi kwa ajili ya usalama wa raia wa DRC