Radio
Zaidi ya watu 30 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na washambuliaji wanaoshukiwa wanajihadi katika mkoa wa Ituri huko DRC
Waasi wa ADF waliwashambulia raia katika vijiji viwili karibu na Komanda umbali wa kilomita 75 na mji wa Bunia alisema David Beiza mkuu wa shirika la Msalaba Mwekundu katika wilaya ya Irumu mkoani Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
Mtoto wa kike akabiliwa na changamoto nyingi kufikia ndoto zake za kielimu
Mkurugenzi wa shirika linato tetea maslahi ya mtoto wa kike nchini Tanzania, Devota Mlay, asema watoto wengi wa kike huacha shule tofauti na wavulana. Matumizi ya wanenguaji wa kike katika harakati za siasa za uchaguzi Kenya yaelezwa kuwa ni moja ya kero na udhalilishaji wa mwanamke.
Tanzania yazindua ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Makutupora mpaka Dodoma
Serekali ya Tanzania imezindua ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Makutupora mpaka Tabora na kuunganisha mataifa ya Rwanda, Burundi, na DRC. Dunia yaadhimisha siku ya mtoto wa mitaani ambapo changamoto kubwa inaelezwa kuwa ni kutoweka msisitizo kwanye shauri hili.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aomba kuhutubia kikao cha Umoja wa Afrika
Wakati Rais Wa Russia Vladmir Putin akisema kwamba mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mzozo kati ya nchi yake na Ukraine yameshindikana, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameomba kuhutubia kikao cha Umoja wa Afrika, kwa mujibu wa rais wa Senegal Macky Sall.