Charles Rubia amemshtaki mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hadj kwa kutowafungulia mashtaka ya ufisadi wanasiasa kabla ya uchaguzi wa Agosti 9.
Uber imetangaza kusitisha huduma zake nchini Tanzania, ikitaja nauli elekezi za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini -LATRA kama sababu ya maamuzi hayo na kudai itarejesha huduma zake kwa nchi hiyo iwapo sheria zitabadilishwa.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Mzozo wa uhaba wa mafuta nchini Kenya unaendelea kutokota licha ya Waziri wa kawi Monica Juma kutangaza hatua kali alizosema zitachukuliwa dhidi ya wanaohodhi bidhaa hiyo huku bei ya mafuta ikiongezwa na mamlaka ya EPRA.