Radio
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aomba vita visitishwe mara moja nchini Ukraine.
Antonio Guteress , akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu Ukraine, amesema jambo la dharura kwa hivi sasa ni kunyamanzisha silaha. Ameomba pia kufanyike uchunguzi huru kuhusu mauaji ya kikatili yanayodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Russia katika mji wa Bucha.
Tunaangazia tuhuma kwamba baadhi ya wasanii wanabuni kashfa ili kujipatia umaarufu na pesa.
Wasanii nchini Kenya waelezea kuridhika kwao na sheria iliyotiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kwamba wanapata hadi asili mia 52 ya ada zinazotozwa wakati sanaa yao inapotumika, tofauti na ilivokuwa awali ambapo walilipwa tu asili mia 16.
Wanawake na watoto waliokimbia mapigano Kivu Kaskazini wapitia hali ngumu
Huko Rutshuru Kivu Kaskazini wanawake na watoto wanaokimbia mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali wanapitia hali mbaya na ngumu ya kimaisha katika shule ambazo zimewahifadhi kwa muda katika Mji wa Rutshuru Kivu Kaskazini.
Ongezeko la bei ya bidhaa nyingine lashuhudiwa Tanzania baada ya mafuta kupanda bei.
Bei ya mafuta imepanda nchini Tanzania huku mfumuko wa bei nchini ukikua kwa wastani wa asilimia 3.7 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2020. Raia tayari wanalalamikia ongezeko kubwa la gharama ya maisha.