Radio
Jaji Ketanji mwanamke wa kwanza mweusi atakayehudumu mahakama ya juu Marekani
Baraza la seneti la Marekani limemuidhinisha Jaji Ketanji Brown Jackson kuwa jaji wa mahakama ya juu ya Marekani kwa kura 53 dhidi ya 47. Baraza la Seneti lilipiga kura Alhamis na kumfanya Jackson mwenye umri wa miaka 51 kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuhudumu katika mahakama ya juu Marekani
Bajeti ya Kenya yakosolewa kwa "kutoangazia vilivyo" maslahi ya wanawake na vijana
Msanii Angel Mary Kato ambaye alitaka kujitoa uhai mara nne anazungumza na Sauti ya Amerika kuhusu changamoto alizopitia na nini anachofanya ili asijipate katika hali kama hiyo tena, huku nayo bajeti ya Kenya ikikosolewa kwa kutoangazia vilivyo maslahi ya wavijana na wanawake.
Mjadala wa Live talk: Siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu Agosti mwaka huu
Vyama vya siasa nchini Kenya kuandaa uchaguzi wa mchujo mwezi huu wa April. Kennes Bwire akishirikiana na Idd Ligongo wanaongoza mjadala wa Live talk, wakiwashirikisha wachambuzi wa siasa Danstan Omar, Koigi Wamwere na Hamisa Zaja