Radio
06:00 - 06:30
Marekani na Uingereza zaomba Russia iondolewe kwenye Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa.
Marekani inasema wakati umewadia kwa Baraza kuu la Umoja wa mataifa kupiga kura ya kuiondoa Russia kwenye Baraza la Umoja wa mataifa la haki za binadamu, kufuatia madai ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa na wanajeshi wa Russia katika mji wa Ukraine wa Bucha.
21:00 - 21:29
Wasiwasi kufuatia ripoti kuwa Waafrika milioni 346 wanakabiliwa na baa la njaa
Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu linasema kwamba robo ya watu wote barani Afrika wanakabiliwa na mzozo mbaya wa njaa kutokana na sababu mbalimbali lakini suala hilo halipewi umuhimu unaostahiki.