Radio
Watu 29 wamejeruhiwa katika shambulizi kwenye kituo cha treni cha Brooklyn huko New York nchini Marekani
Kulingana na maafisa wa jiji la New York mtu mwenye silaha aliyejifunika uso kuzuia moshi wa gesi ya kutoa machozi alifyatua risasi kwenye kituo cha treni cha Brooklyn cha chini ya ardhi na kusababisha hofu miongoni mwa wakaazi ambao ni abiria waliokuwa wakielekea kwenye shughuli mbalimbali za siku
Naibu rais wa Kenya, William Ruto asema kuna hila yeye kutakiwa kuondoka kwenye makazi yake
Naibu rais wa Kenya, William Ruto asema ni hila za kisiasa nyuma ya uamuzi wa kutakiwa aodoke kwenye makazi yake kupisha ukarabati. Wasafirishaji wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam, wasema uceleweshwaji wa mizigo unaweza kuongeza bei ya bidhaa.
Ucheleweshwaji wa mizigo katika bandari ya Dar waibua maoni mseto
Hat baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelezea kutoridhika kwake na uchrleweshwaji wa kupakua mizigo katika bandari ya Dar es Salaam na kuagiza hatua zinazostahili zichukuliwe, wachambuzi wanasema hali hiyo itakuwa na athari ya muda mrefu kwa uchumi wa nchi hiyo.