Radio
Uchaguzi wa awali wa wagombea katika vyama vya Kenya wafanyika
Vijana na wanawake waelezwa kupata uteuzi katika vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu. Ubunifu wa mitindo unaelezwa uaweza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana licha ya kuwa na changamoto. Sababu za wanasichana kutupa ama kutelekeza watoto baada ya kujifungua. Tatizo nini?
Wakristo duniani waadhimisha mateso ya Yesu Kristo katika ibada ya Ijumaa kuu
Wakristo duniani waadhimisha mateso ya Yesu Kristo katika ibada ya Ijumaa kuu na kujiandaa na Pasaka. Makasisi wanasema ni siku muhimu ya kuadhimisha kumbu kumbu ya mateso hayo na wananchi na wachambuzi wa uchumi wanasema imekuja wakati wa hali ngumu ya uchumi.
Waandishi wapiga darubini ripoti kuu wiki hii, zikiwa pamoja na kampuni ya Uber kusitisha shughuli Tanzania
Waandishi kutoka maeneo mbalimbali wanamulika habari kuu za wiki na jinsi zilivyoripotiwa, zikiwa ni pamoja na wasiwasi ulioibuliwa na baa la njaa Afrika Mashariki, mgogoro wa uhaba wa mafuta nchini Kenya na kampuni ya Uber kusitisha shughuli zake nchini Tanzania.