Radio
Idadi ya watu waliofariki kwa mafuriko Afrika kusini imefikia 440
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea Afrika kusini iliongezeka hadi 440 siku ya Jumapili huku mvua ikipungua na kuruhusu shughuli za uokoaji kushika kasi baada ya moja ya dhoruba iliyosababisha vifo zaidi katika kumbukumbu za maisha
Makala ya filamu ya Royal Touri ya utalii wa Tanzania yazinduliwa leo New York,
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anazindua makala ya filamu ya Royal Tour ambayo yeye ndiye mwenyeji akionyesha vivutio vya utalii wa Tanzania. Jamii zatakiwa kuandaa vijana kupinga unyanyasaji wa kijinsia. Binti wa Nigeria azusha gumzo kwenye mitandao ya kijamii akidai kudhalilishwa kijinsia
Makubaliano ya kuwapa hifadhi wahamiaji nchini Rwanda yaibua utata
Makubalinao kati ya Uingereza na Rwanda ambapo wahamiaji wanaojaribu kuingia nchini Uingereza watahamishiwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki yameibua hisia mseto huku baadhi ya wadau, wakiwa ni pamoja na watetezi wa haki za binadamu, wakiyakosoa vikali.