Radio
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa vikosi vya kijeshi vya Burkina Faso, Guinea na Mali kurudisha madaraka kwa raia
ECOWAS iliweka vikwazo vikali dhidi ya nchi ya Mali mwezi Januari baada ya serikali ya kijeshi ilipokataa kurejesha haraka utawala wa kiraia. Imetishia vikwazo kama hivyo dhidi ya Guinea na Burkina Faso kama zitashindwa kuwezesha mpito wa haraka kwa utawala wa kiraia ndani ya muda unaofaa
Waislamu waanza sikukuu ya Eid Ul-Fitr huku wakilalamikia gharama ya maisha
Baadhi ya Waislam katika maneo mbalimbali duniani wameanza kusherehekea Eid Ul-Fitr, sikukuu inayomaanisha kumalizika kwa mfungo baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, wakati ambapo gharama ya maisha imependa kwa kiwango kikubwa.
Wagombea 47 wameidhinishwa Kenya kuwania urais kama wagombea binafsi.
Wagombea 47 wameidhinishwa Kenya kuwania urais kama wagombea binafsi kwenye kinyang’anyiro cha mwezi Agosti mwaka huu, hata pale ambapo vyama vikubwa vya siasa vikizusha vita dhidi ya wanasiasa wanaosimama peke yao gazeti la Daily nation limeripoti.
Kenya, Uganda, Burundi na Misri ni kati ya nchi zilizoanza Sherehe za Eid
Kenya, Uganda, Burundi na DRC ni kati ya nchi za ukanda wa maziwa makuu ambazo tayari zimeanza sherehe za siku tatu za sikukuu ya Kiislamu ya Eid ul-Fitr baada ta mfungo wa Ramadhan huku waumini wengi wakilalamika kuhusu hali ngumu ya maisha.