Radio
Rais Biden amesaini amri ya kiutendaji ambayo italeta uwajibikaji zaidi kwa polisi na sheria ya makosa ya jinai
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amesaini amri ya kiutendaji ambayo anasema italeta uwajibikaji zaidi na ufanisi kwa polisi na sheria ya makosa ya jinai katika kumbukumbuku ya mwaka wa pili wa mauaji ya George Floyd M-marekani mweusi aliyeuawa katika jimbo la Minnnesota na afisa polisi mzungu
Naibu rais wa Kenya William Ruto amemuomba msamaha rais Uhuru Kenyatta baada ya muda mrefu wa kuonekana wakitofautiana kisiasa.
Viongozi hao wawili tangu kuchaguliwa kwa muhula wa pili mwaka wa 2017 walionekana wazi wazi kutoshirikiana kisiasa, wakati mara kadhaa Ruto akidai kupokonywa madaraka , huku naye Kenyatta akidai kwamba naibu wake ameondokea majukumu yake na kujihusisha kwenye kampeni za mapema.
Kibarua kigumu kwa rais mpya wa Somalia kujaribu kuimarisha mahusiano ya kimataifa
Kufuatia kuapishwa kwa rais mpya wa Somalia Hassan Hassan Sheikh Mohamud mapema wiki hii, wachambuzi wanasema ana kibarua kigumu kuwaleta pamoja mahasimu wengi wa kisiasa na kuboresha mahusiano yalyodhoofika kati ya Somalia na baadhi ya majirani wake.