Viongozi hao wawili tangu kuchaguliwa kwa muhula wa pili mwaka wa 2017 walionekana wazi wazi kutoshirikiana kisiasa, wakati mara kadhaa Ruto akidai kupokonywa madaraka , huku naye Kenyatta akidai kwamba naibu wake ameondokea majukumu yake na kujihusisha kwenye kampeni za mapema.