Radio
Spika wa Bunge la Kenya Justin Muturi ametupilia mbali stakabadhi zilizowasilishwa bungeni kuhusu William Ruto na unyakuzi wa ardhi
Mbunge wa jimbo la Wajir Fatuma Gedi aliwasilisha hati za ushahidi bungeni akimhusisha Naibu Rais William Ruto na unyakuzi wa ardhi katika maeneo mbalimbali nchini Kenya huku spika akisema hati hizo zinakosa kukidhi kiwango kilichowekwa na sheria cha kuruhusiwa kukubalika kuwa ushahidi
Wizara ya afya Kenya yataja maambukizi ya VVU yameongezeka miongoni mwa vijana
Mwanaharakati Doreen Moraa Moracha anaeleza kuwa vijana wengi wana taarifa juu ya mapambano na UKIMWI lakini bado wanakosa kupata vifaa kinga ikiwa ni pamoja na mipira ya kondom na hayo yanapelekea maambukizi kuongezeka kati ya umri uliotajwa wa miaka 15 hadi 24.
Polisi wa Kenya wanasa silaha kadhaa huku marufuku ya kutoka nje katika jimbo la Marsabit ikiendelea
Maafisa wa serikali ya Kenya wanasema marufuku iliyowekwa ya kutotoka nje katika jimbo la Marsabit imeanza kuleta tija huku silaha mbaimbali zikinaswa na kupelekea hali ya matumaini ya kuimarisha usalama uliokuwa umezorota.