Radio
16:30 - 17:00
Hisia mseto zatolewa baada ya mwanamke kuteuliwa kuwa mgombe mwenza wa urais nchini Kenya
Bi Martha Karua, ambaye aliwania urais mwaka wa 2013, ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga, anayepeperusha bendera ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, baada ya siku nyingi za mivutano ya kisiasa katika muungano huo.
19:30 - 19:59
Raila Odinga amtangaza mgombea wake mwenza siku moja baada ya William Rutto kufanya hivyo.
Raila Odinga amemtangaza Martha Karua kama mgombea wake mwenza kwa uchaguzi mkuu wa Kenya. Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika imetimiza miaka 60, ni mabadiliko gani yamejitokeza? Ukraine yadai kurejesha nyuma vikosi vya Russia katika eneo la Kharkiv.
21:00 - 21:29
Kiini cha mivutano ya mara kwa mara kuhusu madini ya Afrika Mashariki na Kati na sulihisho lake
Changamoto za uchimbaji wa madini katika ukanda wa Afrika Mashariki zimekuwa donda sugu kwa miongo kadhaa sasa huku mingi ya mikataba inayotiwa saini na wadau ikiendelea kuibua utata mkubwa. Nini kiini cha mizozo hii na inaweza kutatuliwaje?