Radio
06:00 - 06:30
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud anaanza muhula wake wa miaka minne akikabiliwa na changamoto kuu ya kisiasa
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud anaanza muhula wake wa miaka minne akikabiliwa na masuala makuu yanayojulikana ikiwemo mgawanyiko wa kisiasa nchini humo na kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na kundi la uasi la Al-Shabaab lenye uhusiano na al-Qaida
16:30 - 16:59
Vijana nchini Uganda wamkosoa Rais Museveni "kwa kutochukua hatua za kuimarisha hali ya maisha"
Kufuatia hotuba ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni jana Jumapili, ambapo alisema hakuna uwezekano wowote wa punguza kodi, aili kupunguza athari za kupanda kwa gharama ya maisha, baadhi ya vijana nchini humo wanasema hawana matumaini ya kuimarisha hali yao ya maisha katika mazingira ya sasa.