Radio
06:00 - 06:29
Polisi wa Somalia anasema watu saba walijeruhiwa Jumatano katika shambulizi la kujitoa mhanga
Msemaji wa polisi nchini Somalia Abdifatah Adan Hassan aliwaambia waandishi wa habari mlipuko wa kujitoa mhanga karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu ambalo ni eneo la uchaguzi wa Rais siku ya Jumapili umejeruhi watu saba
16:30 - 16:59
Wanawake wa Kenya wakosoa uamuzi wa mahakama kuhusu agizo la IEBC la uteuzi wa anagalau theluthi moja ya wanawake
Kufuatia hatua ya mahakama kuu ya Kenya Alhamisi kusitisha maagizo ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, yakivitaka vyama vya kisiasa kuteua angalau theluthi moja ya kila jinsia, baadhi ya wanawake wamekosoa uamuzi huo kama usiotilia maanani umuhimu wa kuiwezesha jinsia ya kike.
21:00 - 21:29
Tanzania: Wanawake 19 waliovuliwa uanachama na chama cha Chadema wapuzilia mbali hatua hiyo
Hatua ya kutupilia mbali rufaa ya wanawake 19 waliovuliwa uanachama na chama cha upinzani cha Tanzania, Chadema, imetajwa na baadhi yao kama ya kiuhuni huku naye mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akisesema wao ndio wahuni.