Radio
06:00 - 06:30
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya juu ya njaa nchini Somalia na kuongezeka kwa vifo vya watoto katika Pembe ya Afrika
Pembe ya Afrika inashuhudia mwaka wake wa nne mfululizo kwa kushindwa kupata mvua tukio la hali ya hewa ambalo halijaonekana kwa angalau miaka 40. Kama ukame utaendelea shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kwamba watu milioni 20 watakabiliwa na njaa kali mwishoni mwa 2022
16:30 - 16:59
Visa vya ukatili wa kingono dhidi ya watoto pamoja na mauaji ya wapenzi na wanandoa vimeongezeka sana katika siku ya karibuni.
Kutokana na hali hiyo maafisa wa Ustawi wa Jamii kutoka Mwanza wamezindua program ya kuhamasisha wanafunzi kuhusu usalama wao na namna ya kuwasilisha ripoti iwapo wako hatarini.
21:00 - 21:29
KWA UNDANI: Mazungumzo namna ya kusafirisha chakula kutoka Ukraine hadi katika masoko ya kimataifa hasa Afrika na mashariki ya kati
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.