Wakati June 16 ni siku ya mtoto wa Afrika, watoto na wanaharakati wa haki za watoto nchini Kenya, waitaka serikali kuzingatia changamoto zinazowakabili watoto, hasa wakati huu ambapo nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Mkurugenzi wa mtandao wa East Afrika Child Network anasema mtandao ambao unashughulikia haki za watoto katika nchi za Afrika mashariki na kati anaeleza mtoto wa Afrika ana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na usalama wake, elimu na anahitaji kulindwa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ni kati ya viongozi waliozuru Ukraine na kuahidi msaada zaidi wa silaha na uungwaji mkono wa azma ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa ulaya.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.