Radio
06:00 - 06:30
Mwana Mfalme Mohammed bin Salman (MBS) amekutana rasmi na viongozi wa Misri, Jordan na Uturuki ili kuimarisha mahusiano ya usalama ulioyumba
Wachambuzi wanasema hii inaashiria pia azma ya MBS kutambuliwa katika jukwaa la ulimwengu na kumaliza miaka kadhaa ya kutengwa kimataifa kufuatia mauaji ya mwaka 2018 ya mkosoaji wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi mjini Istanbul, ambapo mkuu huyo amekanusha kuhusika binafsi
16:30 - 16:59
Wanawake na watoto waliokimbia makwao DRC waomba usaidizi
Mashirika ya kutetea haki za raia mashariki mwa DRC yanasema yana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya wanawake na watoto waliofurushwa makwao kutokana na mapigano kati ya waasi na jeshi wanaishi maisha duni na kuna haja ya kuwapa msaada wa dharura.
21:00 - 21:30
KWA UNDANI: Maoni ya waandishi wa habari kuhusu habari kuu wiki hii ikiwemo mapigano DRC na mgomo wa walimu Uganda
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.