Radio
06:00 - 06:30
Rais kenyatta wa kenya anatarajiwa kuongoza mkutano wa marais juu ya kuleta amani DRC
Viongozi hao wanatarajiwa pia kuafiki utaratibu wa kupeleka jeshi la kikanda ili kurejesha amani Mashariki mwa DRC. Haya yanajiri siku moja baada ya makamanda wa majeshi ya jumuiya hiyo kukutana Nairobi kuafikiana kuhusu mfumo wa kupeleka kikosi cha kijeshi cha EAC nchini DRC
19:30 - 19:59
Madaktari, wauguzi na walimu wa Zimbabwe waanza mgomo kulalamikia mishahara duni.
Wafanyakazi hao wanasema kwamba dhamani ya fedha imeshuka kiasi cha mishahara yao kutoweza kumudu gharama ya maisha. Hayo yamejiri licha ya ahadi ya mwezi uliopita kutoka kwa serikali kwamba mishahara ingeongezwa maradufu.