Radio
06:00 - 06:30
Serikali ya Libya na makundi ya upinzani yanashutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu inaeleza ripoti ya wachunguzi kutoka UN
Hii ni ripoti ya tatu ya tume huru inayoangazia ukweli kuhusu Libya tangu ilipoanza kuandika madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo mwaka 2016. Wachunguzi wanaona kwamba Libya ni nchi isiyoheshimu sheria ambapo wahalifu wa uhalifu wa kimataifa hawawajibiki kwa matendo yao.
16:30 - 17:00
Msanni kutoka Tanzania Maalim Nash au Nash MC atembelea studio za VOA Express
Nash MC anasema kwamba miongoni mwa sababu zilizomleta Marekani ni pamoja na kukuza sanaa ya hiphop, kukuza lugha ya kiswahili kwenye sanaa, pamoja na kuhakikisha kwamba muziki wa Afrika mashariki unafikia viwango vya kimataifa.
19:30 - 20:00
21:00 - 21:29
Kwa Undani: Kagame na Tshisekedi kukutana Angola huku Rwanda ikisisitiza kwamba DRC ishughulikie matatizo yake bila kuihusisha na M23
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.