Maandalizi yanaendelea juu ya kutoa chanjo ya kwanza ya malaria duniani kwa watu wengi, chanjo iliyofadhiliwa na mpango wa GAVI kwa dola milioni 160 kulinda mamilioni ya watoto barani Afrika.
Mabinti wa shule za kutwa wametaja mimba za utotoni na kuchelewa shule ni moja ya changamoto zao kubwa kutokana na shida ya usafiri kuelekea na kutoka shuleni.
Watalaam wa hali ya hewa na majanga kutoka nchi za Kenya na Tanzania wahimiza kuwe na vitendo zaidi na wanasiasa kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki wafanyika Arusha. Rais Putin akutana na Marais wa Iran na Uturuki. Sri Lanka yapata rais mpya baada ya maandamano makubwa. Mashindano ya riadha ya dunia yakamilika, Afrika mashariki yatamba.