Mamia ya wafuasi wa kiongozi wa kidini Muqtada al-Sadr waliingia katika jengo la bunge jumamosi kwa mara ya pili wiki hii. Mapema, vikosi vya usalama vya Iraq vilipambana na maelfu ya waandamanaji huko Baghdad katika eneo linalojulikana kama Green zone.