Radio
WHO: Umri wa kuishi barani Afrika waongezeka
Takwimu mpya katika ripoti ya WHO ya Alhamisi zaonyesha kuwa umri wa kuishi barani Afrika umeongezeka kwa karibu miaka 10 kati ya mwaka wa 2000 na 2019. Kinachoonekana zaidi katika ripoti hiyo ni kuongezeka kwa umri wa kuishi kutoka miaka 46 mwaka wa 2000 hadi miaka 56 mwaka wa 2019.
Mfanyabiashara nchini Marekani kutoka Tanzania aeleza mafanikio na changamoto zake.
Mfanyabiashara wa vyakula Janet Gabagamu mmiliki wa Joy Catering aliyeko Minnesota, anasema mapenzi yake katika mapishi yalimwingiza katika biashara hiyo. Na anaeleza changamoto zilizopo kama mfanyabiashara Mhamiaji nchini Marekani.
Jioni: Mjadala kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya wenye ushindani mkali kati ya William Ruto na Raila Odinga
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.